BURUNDI-USWISI

Mwili wa mfalme Mwambutsa IV kutorejeshwa nchini Burundi

Mfalme Mwambutsa IV mwaka 1962.
Mfalme Mwambutsa IV mwaka 1962. CC/Fritz Cohen

Baada ya miaka minne ya vita vya kisheria nchini Uswisi, mahakama ya mjini Geneva hatimaye imeamua kwamba mabaki ya Mfalme Mwambutsa IV hayatarejeshwa nchini Burundi.

Matangazo ya kibiashara

Mwili wa Mfalme wa zamani, aliyesafirishwa nchini Uswisi na mtoto wake mwaka 1966, utabaki katika nchi ya Uswisi iliyompokea. Mfalme Mwambutsa IV alifariki dunia waka 1977. Lakini miaka minne iliyopita, utaratibu wa kurudisha mwili wa Mfalme nchini Burundi ulizinduliwa.

Mwili wa mfalme Mwambutsa IV ulifukuliwa kutoka kaburi alikozikwa mwaka 2012 kwa ombi la binti yake, na kuungwa mkono na serikali ya Burundi ambayo ilikua ikiandaa miaka hamsini ya uhuru. Hoja iliyotolewa na serikali ya Burundi ni kwamba kurejeshwa kwa mwili wa Mfalme Mwambutsa IV kunaweza kusaidia mchakato wa maridhiano nchini na kuchangia kupunguza mvutano wa kisaiasa.

Hoja hii ilifutiliwa mbali na mpwa wa Mfalme Mwambutsa, Princess Esther Kamatari. "Hii ni hoja ambayo haieleweki kabisa kwani hata mahakam iliweza kuthibitisha kwamba kulikuwa hakuna umuhimu wa mtu aliyefariki kwenda kupatanisha watu nchini Burundi, Princess Esther Kamatari ameelezea. Haiwezekani wafu kupatanisha watu hai. Mfalme Mwambutsa alisema yale yanayoweza kutokea, kutumia mabaki yake kwa mambo ya kisiasa, na nadhani alikuwa na ufahamu sana. "

Mfalme Mwambutsa IV alisema na aliandika kabla ya kufa kwake: 'Naeleza kile kilicho moyoni kwamba mwili wangu usizikwe mahali pengine ispokua Uswisi, usirejeshwi nchini Burundi au katika nchi nyingine yoyote.' Kauli hii ya Mfalme Mwambutsa IV umezingatiwa na mahakama ya Uswisi, labda kesi bado haijamalizika. Rufaa inawezekana katika mahakama ya Uswisi, amesema Princess Kamatari.