KENYA-UN

Kenyatta aituhumu UN kushindwa kutekeleza wajibu wake

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, aulaumu Umoja wa Mataifa kushindwa kutekeleza majukumu yake nchini Sudana Kusini.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, aulaumu Umoja wa Mataifa kushindwa kutekeleza majukumu yake nchini Sudana Kusini. State House Kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ameushtumu Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo nchini Sudan Kusini na badala yake kuamua kumfuta kazi aliyekuwa Kamanda wa jeshi la kulinda amani nchini humo, ambaye ni raia wa Kenya Luteni Jenerali Johnson Ondieki.

Matangazo ya kibiashara

Kenyatta ameongeza kuwa, Umoja wa Mataifa unakimbia majukumu yake nchini Sudan Kusini na sasa serikali yake imeamua kuwarudisha nyumbani wanajeshi wake zaidi ya 1000 ambao wamekuwa nchini Sudan Kusini.

Katika hatua nyingine, Mwakilishi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Macharia Kamau ameushtumu Umoja huo kwa kukubali shinikizo ya mataifa kadhaa ya Baraza la Usalama, kumfuta kazi Kamanda huyo nchini Kenya lakini Urusi imeshtumu uamuazi huo.

Katibu Mkuu Ban Ki Moon tayari amemteua Meja Jenerali Chaoying Yang, kutoka nchini China kuongoza kikosi hicho cha Umoja wa Mataufa nchini Sudan Kusini.

Itakumbukwa kwamba Alhamisi wiki hii Umoja wa Mataifa ulimteua afisa wa jeshi la China kukaimu nafasi aliyokua akishikilia Luteni Jenerali Johnson Ondieki.