Habari RFI-Ki

Bunge lapitisha muswada wa sheria ya habari nchini Tanzania,waandishi wasemaje?

Sauti 10:02

Bunge nchini Tanzania mwishoni mwa juma limepitisha muswada wa sheria ya hhuduma za habari wa mwaka 2016 tayari kusainiwa na raisi ili kuwa sheria kamili.Hata hivyo wadau wa habari na wanahabari wamelalamikia kupitishwa kwa muswada huo kuwa sheria kwa madai kuwa hawakupewa muda kujadili masuala kadhaa yaliyomo ndani ya muswada huo kwa lengo la kufikia makubaliano ya pamoja.Juma lililopita raisi wa Tanzania John Magufuli alisema hatasita kutia saini muswada huo kuwa sheria,mara utakapofika mezani kwake.Tunazungumza na wadau wa habari kujua manufaa ya sheri ahiyo na changamoto mara itakapoanza kutumika.