SUDAN KUSINI

Watu 11 wauawa wakitazama mechi Sudan Kusini

Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini ambapo watu 11 waliuawa na mtu aliyewafyatulia risasi walipokua wakitazama mechi ya ligi ya Premia, Jumapili Novemba 6, 2016.
Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini ambapo watu 11 waliuawa na mtu aliyewafyatulia risasi walipokua wakitazama mechi ya ligi ya Premia, Jumapili Novemba 6, 2016. REUTERS/Stringer

Hali ya sintofahamu ilitokea siku ya Jumapili Novemba 6 nchini Sudan Kusini ambapo watu 11 waliuawa na wengine 16 kujeruhiwa baada ya mtu mwenye bunduki kufyatulia risasi watu waliokuwa wakitazama mechi ya Ligi ya Premia katika mji wa Gure ulio karibu namji wa Juba, mashahidi wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Polisi inasema wameanzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo, lakini mpaka sasa hawajajua kilichosababisha mauaji hayo.

Gazeti la National Courier linasema mtu aliyetekeleza mauaji hayo alifanikiwa kutomka baada ya kitendo hicho kiovu, licha ya polisi kufika eneo haraka eneo la tukio.

Itafahamika kwamba hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa katika mji mkuu wa Sudan Kusini kwa muda wa miezi minne sasa tangu machafuko kuukumba mji huo mwezi Julai baada ya wanajeshi wa Rais Salva Kiir kukabiliana na wale wa Riek Machar, na kupelekea Bw. Machar kukimbilia katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Katika mapigano hayo watu kadhaa waliuawa ikiwa ni pamoja na askari kutoka pande mbili.