UGANDA-BESIGYE-SIASA

Besigye aondoka nchini Uganda

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ameitoroka nchi yake. Hayo ameyathibitisha mwenyewe kwenye mtandao wa twitter kuwa ameondoka nchini humo.

askari polisi wa Uganda wakipiga kambi mbele ya makazi ya mpinzani mkuu Kizza Besigye,Februari 22,2016, katika moja ya vitongoji vya mji wa Kampala.
askari polisi wa Uganda wakipiga kambi mbele ya makazi ya mpinzani mkuu Kizza Besigye,Februari 22,2016, katika moja ya vitongoji vya mji wa Kampala. Isaac Kasamani / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Kizza Besigye akinukuliwa na gazeti la Daily Monitor Jumatatu wiki hii kuwa, aliamua kufuta safari yake kwenda nchini Afrika Kusini siku ya Jumanne kufuatia hatua ya polisi ya kuweka kizuizi nje ya nyumba yake.

Serikali imekua ikijaribu kumzuia ili asiondoki bila mafanikio, amesema Bw. Besigye.

Hata hivyo msemaji wa polisi alikanusha madai hayo, akisema kuwa ni mbinu za Kizza Besigye kutaka kuonyesha kuwa hatendewi haki wakati sivyo.

Kizza Besigye anatarajiwa kuhutubia mkutano wa tume ya kimataifa ya mawakili mjini Johannesburg siku ya Alhamisi.