SUDANI KUSINI

UN yahofia kuenea mapigano ya kikabila Sudan Kusini

Baadhi ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wakiwa katika kambi ya Ayilo nchini Uganda
Baadhi ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wakiwa katika kambi ya Ayilo nchini Uganda Flick'r/CC

Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa wa masuala ya kuzuia mauaji ya halaiki Adama Dieng, ameelezea wasiwasi wake juu ya kuenea kwa ghasia za kikabila nchini Sudan Kusini,wakati huu umoja wa ulaya EU ukitoa msaada wa dharura kwa wakimbizi.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza huko Yumbe jirani na nchi ya Uganda, kamishna wa misaada ya kibinadamu katika umoja wa ulaya alitoa kiasi cha Euro milioni 78 ili kuwasaidia wakimbizi na milioni 30 zilizotengwa kwa ajili ya Uganda.

Christos Stylianides amesema ameshtushwa na hali aliyoiona na kuongeza kuwa anafikiri hali halisi inachukuliwa katika kiwango cha chini,wakati uhitaji ni mkubwa na unaongezeka.

Uganda,kwa sasa inahifadhi takribani wakimbizi laki tano na thelathini,ambapo wakimbizi wa Sudani kusini ni laki tatu na thelathini ambao walikimbia mapigano kwa mwaka huu pekee.