KENYA-UN

Kenya yakataa kushirikiana na UN Sudan Kusini

Serikai ya Kenya imetangaza kwamba iko tayari kuisaidia nchi changa ya Sudan Kusini kuimarisha usalama wake bila kushirikiana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS.

Rais wa Kenya  Uhuru Kenyatta Makamu wake William Ruto Aprili 4, 2015 mjini Nairobi.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Makamu wake William Ruto Aprili 4, 2015 mjini Nairobi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya askari wa Kenya waliokuwa wakihudumu nchini Sudan Kusini katika jimbo la Wau wamerudishwa nyumbani tangu wiki iliyopita.

Kenya iliondoa vikosi vyake kutoka nchini Sudan Kusini kufuatia uamuzi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kumuachisha kazi afisa wake, Johnson Ondieki, aliyekuwa akiongoza kikosi cha Umoja wa Matifa nchini Sudan Kusini (UNMISS).

Msemaji wa serikali Manoah Esipisu amesema kuwa Kenya itashirikiana na Sudan Kusini kupitia mashirika mbalimbali lakini haitasitisha msimamo wake wa kuondoa wanajeshi wake nchini humo.

“Hatua ya UNMISS kushindwa kuishauri Kenya kuhusu hatua yake ya kumfuta kazi Luteni jenerali Johnson Ondieki inaonyesha ukosefu wa heshima kwa Kenya”, amesema msemaji wa serikali Manoah Esipisu.

Hata hivyo upinzani nchini Kenya umeikosoa serikali kwa kuchukua hatua hiyo ukibaini kwamba utaisababishia madhara nchi hiyo.