Burundi: Serikali yakashifu ripoti ya shirika la FIDH, lenyewe laonya uwezekano wa kutokea mauaji

Waandamanaji raia wa Burundi wakiwa kwenye jiji la Bujumbura, 24 Septemba 2016.
Waandamanaji raia wa Burundi wakiwa kwenye jiji la Bujumbura, 24 Septemba 2016. Tony KARUMBA / AFP

Shirikisho la kimataifa la haki za binadamu, FIDH, linaituhumu Serikali ya Burundi na vyombo vyake vya usalama, kuendelea kutekeleza vitendo vya kikatili dhidi ya raia na kuonya kuwa huenda nchi hiyo ikashuhudia mauaji ya kimbari.

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limesema kuwa, toka mwezi April mwaka 2015 ambapo ndio kulizuka maandamano ya raia kupinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza, nchi ya Burundi imejikuta ikutumbukia kwa machafuko ya kisiasa.

"Lazima tuzuie matukio haya ambayo yamekuwa ni yakikatili," amesema rais wa shirika hilo Dimitris Christopoulos, ambapoa akaongeza kuwa "hebu tuchukue hatua kabla hatujachelewa."

Katika ripoti yake yenye kurasa 200, shirika hilo limeonesha namna ambavyo Serikali ya Burundi imefadhili machafuko yaliyoshuhudiwa nchini humo wakati wa kampeni ya kupiga vita makundi yanayodaiwa kuchochea vurugu nchini humo.

"Msako unaofanywa na vyombo vya usalama na pia kuhusika kwa kundi la vijana wa chama tawala Imbonerakure...malengo yao yamekuwa ni kung'ang'ania madarakani kwa kutumia kila aina ya mbinu,"

Zaidi ya watu elfu 1 wamekufa na wengine zaidi ya 800 hawajulikani walipo, imesema ripoti hiyo iliyopewa jina "Ukandamizaji na Mauaji ya halaiki nchini Burundi".

Watu wanaokadiriwa kufikia elfu 8 wanashikiliwa kwa sababu za kisiasa na wengine zaidi ya laki 3 wamelazimika kuikimbia nchi yao.

FIDH limesema kuwa ripoti hiyo inatolewa baada ya uchunguzi wao wa miaka takriban miwili kuhusu tuhuma za unyanyasaji wanaofanyiwa raia na vyombo vya usalama nchini humo.

Hata hivyo, Serikali ya Burundi, imetupilia mbali ripoti ya FIDH, ikisema imejaa uchochezi na upendeleo mkubwa kwa wale wanaodaiwa na Serikali kuwa wamekuwa wakichochea na kufanya vitendo vya kihalifu nchini humo.

The FIDH, along with leading Burundian rights group the ITEKA League, spent two years investigating rights abuses in the country.

"All the criteria and conditions for the perpetrating of genocide are in place," the report said, listing "ideology, intent, security institutions... identifying populations to be eliminated, and the using of historical justifications."

Burundi suffered a brutal civil war from 1993 until 2006 between majority Hutus and minority Tutsis, which claimed an estimated 300,000 lives.

A failed coup in May 2015 was the "breaking point" after which the authorities adopted a "logic of systematic repression", the report said.