BURUNDI-UBELGIJI-USHIRIKIANO

Burundi yaitwika lawama Ubelgiji

Makao makuu ya chama cha madarakani, CNDD-FDD mjini Bujumbura.
Makao makuu ya chama cha madarakani, CNDD-FDD mjini Bujumbura. AFP PHOTO/PHIL MOORE

Jumatatu hii Novemba 21 Bunge la Ubelgiji litapokea ujumbe wa mashirika ya kiraia kutoka Burundi yaishiyo uhamishoni. Mada ambayo itazungumziwa ni : "Kitu gani kinachozuia jamii ya kimataifa kuchukua hatua na kuwalinda raia wa Burundi? ".

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Burundi ambayo inashtumu mashirika hayo kuhusika katika jaribio la mapinduzi la Mei 2015, haikufurahia mwaliko huo wa Bunge la Ubelgiji kwa mashirika hayo ya kiraia yaishiyo uhamishoni. Katika siku za hivi karibuni, chama tawala, mashirika ya kiraia yalio na uhusiano wa karibu na chama hicho na hata Baraza la Seneti waliendelea kuinyooshea kidole cha lawama Ubelgiji.

"Walowezi ndio walitugawanya na kuchochea chuki kati ya jamii nchini Burundi," amesema katibu mkuu wa CNDD-FDD katika ufunguzi wa wiki ya sikukuu kwa wapiganaji iliyoandaliwa na chama tawala. Katika shutma hizo za maneneo makali, Baraza la Seneti, katika barua lililoliandika Bunge la Ubelgiji, limelilaumu kualika watu lililowataja "wahalifu" na "wenye hatia ya uhalifu usiyo na kifani."

Watu hawa ni viongozi wa vyama vya kiraia kutoka Burundi waishio kwa sasa uhamishoni. Pia viongozi hao wanalengwa na mshirika yalio na uhusiano wa karibu na serikali. Serikali na mashirika hayo walikutana Ijumaa ili kukemea kile walichokiita 'Jukumu la Ubelgiji katika historia ya kusikitisha ya Burundi na kuhatarisha amani.'

Mwishoni mwa barua yake, Baraza la Seneti la Burundi limeomba kutumwa nchini Burundi 'ujumbe wa taarifa za kweli ili wabunge watoe wazo lao wenyewe kuhusu nchi yao.

Mwaliko unaoshangaza kwa serikali ya Bujumbura, kwani inakataa katu katu kutumwa kwa askari polisi 228 wa Umoja wa Mataifa. Itakumbukwa kwamba serikali ya Burundi hakusaini mkataba kwa ajili ya kutumwa nchini Burundi waangalizi wa Umoja wa Afrika AU, na hivi karibuni ilitangaza kutukua na imani na wataalam wa Umoja wa Mataifa.