BURUNDI-MSULUHISHI-SIASA

Edouard Nduwimana, Msuluhishi mpya wa taifa nchini Burundi

Edouard Nduwimana, Naibu wa pili wa Spika wa Bunge la Burundi, achaguliwa kuwa Msuluhishi wa taifa.
Edouard Nduwimana, Naibu wa pili wa Spika wa Bunge la Burundi, achaguliwa kuwa Msuluhishi wa taifa. assemblee.bi

Siku moja baada ya Mohammed Khalfan Rukara kutoa hotuba ya kutangaza na kuwaaga wananchi wa Burundi kwamba muda wake wa kuhudumu kama Msuluhishi wa kitaifa umefikia tamati, hatimaye Jumatatu hii Bunge na Baraza la Seneti vya Burundi vimempitisha Edourad Nduwimana kushikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka 7.

Matangazo ya kibiashara

Edouard Nduwimana, Naibu wa pili wa Spika wa Bunge amepitishwa kuwa Msuluhishi mpya wa taifa kwa 91.3% ya kura. Amechukua nafasi ya mtangulizi wake Mohammed Khalfan Rukara, ambaye ametangaza Jumapili hii kuwa amemaliza muhula wake wa miaka saba.

Nafasi ya Naibu wa pili wa Spika wa Bunge, amechaguliwa Jacky Chantale Nkurunziza kwa kura 111 dhidi ya mbili. Bii Jacky Chantale anachukua nafasi ya Edourad Nduwimana.

Edouard Nduwimana ni kutoka jamii ya Watutsi, licha ya kushirikiana kwa kipindi kirefu na mfuasi katika safa ya mbele wa chama tawala cha CNDD-FDD.

Mashirika kadhaa ya haki za binadamu nchini Burundi, hata baadhi ya wadadisi walikoa wakikosoa mwenendo wa Edourd Nduwimana alipokua Waziri wa Mambo ya Ndani (zaidi ya miaka 7 iliyopita) kabla ya kuchukua nafasi ya Naibu wa pili wa Spika wa Bunge, mwishoni mwa mwaka 2015, hasa kwa sheria alizokua akichukua dhidi ya upinzani na mashirika ya kiraia, bila kusahau uamuzi wa kuifunga radio RPA mwanzoni mwa mwaka 2015 kwa faida ya utawala wa Pierre Nkurunziza.

Mshauri mkuu wa rais Pierre Nkurunziza, anayehusika na masuala ya mawasiliano, Willy Nyamitee ambaye, anadaiwa na upinzani pamoja na vyama vya kiraia vilio uhamishoni kuwa ni mtu mwenye ushawishi mkubwa katika chama cha CNDD-FDD, ameandika kwenye twiterr akipongeza kupitishwa kwa Edouard Nduwimana kama Msuluhishi mpya wa taifa.

Edouard Nduwimana anatazamiwa kutawazwa Jumanne wiki hii mbele ya Bunge na Baraza la Seneti.