UNESCO-UGANDA

UNESCO yatambua muziki wa asili aina ya Ma'di nchini Uganda

Muziki wa asili Ma'di nchini Uganda ambao ulikuwa umeanza kutoweka, umehifadhiwa rasmi katika rekodi ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).

Nembo ya UNESCO
Nembo ya UNESCO Unesco
Matangazo ya kibiashara

Pamoja na muziki na utamaduni huo, Muziki aina ya Cossack kutoka Ukraine na sanaa ya ufinyanzi kutoka nchini Ureno imehifadhiwa na Shirika hilo.

Uamuzi huu umefikiwa wakati wa mkutano wa Kamati ya UNESCO, iliyokutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia siku ya Jumanne wiki hii.

Muziki wa kiasili wa Uganda wa Ma'di kutoka kwa jamii ya Ma'di itahifadhiwa katika makao makuu ya Shirika hilo jijini Paris nchini Ufaransa na kukumbukwa kwa miaka nyingi ijayo.

Lengo la hatua hii ni kuhifadhi tamaduni za zamani ambazo zinaonekana kusahaulika katika miaka ya hivi karibuni ili kutoa elimu na historia ya maswala mbalimbali.