RWANDA-UKIMWI

Hatua kubwa yapigwa nchini Rwanda katika kupambana dhidi ya Ukimwi

Katika mtaa mmoja mjini Kigali, Rwanda.
Katika mtaa mmoja mjini Kigali, Rwanda. RFI/Stéphanie Aglietti

Nchini Rwanda, sera za umma katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi inaonekana kuzaa matunda, kulingana na takwimu zinazotolewa na serikali ya nchi hiyo. Miongoni mwa hatua zilizotekelezwa, usambazaji wa kondomu za bure katika vibanda mbalimbali. Watu wanakuja kuchukua kodomu hizo wanakua hawana wasiwasi, na kufurahia huduma hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Rwanda kwa miaka mingi imekua ikipambana dhidi ya ugojwa wa Ukimwi. Kwa mujibu wa UNAIDS katika mwaka 2014 nchini Rwanda, zaidi ya 95% ya wanawake wajawazito wenye VVU walipata dawa za kupunguza makali ya Ugonjwa huo nakuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Kampeni nyingi za kuzuia ugonjwa huo zinaendeshwa na serikali. Kiwango cha taifa cha maambukizi kimeshuka hadi 3%. Hata hivyo, kiwango hiki kiko juu katika mji wa Kigali kwani kinafikia 6.3%. Tangu mwezi Mei, serikali ya Rwanda, ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Marekani, ilitenga vibanda katika mji mkuu wa Rwanda ambavyo vinatoa kondomu za bure kwa watu ambao wanataka kuzitumia.

Hata hivyo wasichana walioambukizwa virusi hivyo wanasema wameendelea kunyanyapaliwa hasa wanapotaka kuolewa.

WHO inasema watu Milioni 36.7 kote duniani wanaishi na ugonjwa huu lakini nusu ya watu hao hawafahamu ikiwa wameambukizwa.

Bara la Afrika linaendelea kuongoza kwa maambukizi ya virusi hivi, huku matumizi ya dawa ya kupunguza makali ya virusi hivyo ARV zikisalia kuwa changamoto kwa baadhi ya watu.