KENYA

Upinzani nchini Kenya wamshtumu rais Kenyatta kwa matamshi ya uchochezi

Raila Odinga, kiongozi wa chama cha ODM nchini Kenya
Raila Odinga, kiongozi wa chama cha ODM nchini Kenya REUTERS/Noor Khamis

Chama Kikuu cha upinzani nchini Kenya ODM, kimemshtumu rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kwa kutoa matamshi ya uchochezi.

Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa chama hicho John Mbadi amesema ikiwa viongozi hao hawataacha uchochezi huo, watazua mzozo wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Aidha, amezishtumu taasisi za serikali kwa kutozungumzia suala hili na kuchukua hatua yeyote kwa mujibu wa sheria.

“Lugha inayotumiwa na rais Kenyatta na Naibu wake, inaipeleka nchi hii pabaya,” alisema Mbandi kupitia taarifa aliyoituma kwa vyombo vya Habari.

Matamshi haya yanakuja baada rais Kenyatta kumshutumu kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga kwa kusema uongo kuhusu madai ya ufisadi yanayoikumba serikali yake.

Kenyatta amemtaka Odinga kujiuzulu siasa na kuacha kuikosoa serikali yake hata kama hakuna cha kumkosoa.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao, wachambuzi wa siasa wanaonya kuwa matamshi kama haya yakiendelea huenda yakaanza kuzua wasiwasi wa kisiasa.