SUDAN KUSINI-TANZANIA

Mjane wa John Garang akutana na Rais Magufuli

Maelfu ya raia waliokimbilia kanisani mjini Juba, wakikimbia ghasia zilizozuka katika mji mkuu wa Sudan Kusini.
Maelfu ya raia waliokimbilia kanisani mjini Juba, wakikimbia ghasia zilizozuka katika mji mkuu wa Sudan Kusini. Peter MARTELL / AFP

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amekutana kwa mazungumzo na Rebecca Nyandeng Garang Mabior, mjane wa John Garang, Mwanzilishi wa Taifa la Sudan Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mkutano huo Bi Mabior, amekuja nchini Tanzania kukutana kwa mazungumzo na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya afrika ya Mashariki kwa lengo la kumfahamisha hali inayojiri wakati huu nchini Sudan Kusini.

Bi Mabior na ujumbe wake wamemuomba Rais Magufuli na viongozi wenzake wa jumuia ya Afrika ya Mashariki kufanya kilio chini ya uwezo wao ili kuisaidia nchi Sudan Kusini kutafutia ufumbuzi mgogoro unaolikabili taifa hilo changa barani Afrika.

Rais Magufuli kwa upande wake amewasihi viongozi na wananchi wa Sudan ya Kusini kutafuta njia muafaka ya kupatia ufumbuzi tofauti zao kwa njia ya amani na kuepuka machafuko yanayosababisha mateso kwa wananchi wa Taifa hilo.