Kenya

Lori la mafuta lalipuka Naivasha Kenya laua zaidi ya watu 30

Lori la mafuta likiwaka moto baada ya kugonga tuta na kuhama njia huko Naivasha Kenya
Lori la mafuta likiwaka moto baada ya kugonga tuta na kuhama njia huko Naivasha Kenya http://www.theorion.co.ke/

Zaidi ya watu 30 wamepoteza maisha baada ya lori la mafuta kugonga magari mengine na kulipuka nje ya mji wa Naivasha nchini Kenya usiku wa jana Jumamosi, maafisa wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza mapema leo asubuhi msemaji wa idara ya taifa ya mambo ya dharura nchini Kenya Pius Masai amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba magari zaidi ya 11 yameteketezwa kwa moto katika barabara ya Nairobi-Naivasha.

Aidha Masai ameongeza kuwa hadi saa kumi na moja alfajiri idadi ya vifo ilikuwa imefikia watu 33 lakini utafutaji wa manusra na miili mingine bado unaendelea na idadi huenda ikaongezeka.

Maafisa kutoka wizara ya usafirishaji wakiongozwa na Katibu mkuu wa wizara hiyo Irungu Nyakera wamewasili katika eneo la tukio na Taarifa zaidi zinaeleza kuwa watu wengi wamejeruhiwa na miongoni mwao ni watu waliokuwa wakirejea nyumbani kutoka harusini subukia.

Katibu mkuu  Irungu amesema kuwa kwa utafiti wa awali umebaini kuwa ajali hiyo imetokana na dereva kutokufahamu vizuri barabara hiyo kutokana na kwamba lori hilo la mafuta ni la nchini Uganda.