KENYA-UHURU

Kenya yaadhimisha miaka 53 ya uhuru wake

Gwaride na michezo mbalimbali ikitazamiwa kushuhudiwa Jumatatu Desemba 12 hii mjini Nairobi, kwa maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Kenya.
Gwaride na michezo mbalimbali ikitazamiwa kushuhudiwa Jumatatu Desemba 12 hii mjini Nairobi, kwa maadhimisho ya miaka 53 ya uhuru wa Kenya. Reuters/Noor Khamis/File Photo

Kenya inaadhimisha miaka 53 ya Uhuru Jumatatu hii. Siku kama ya leo mwaka 1963, nchi hiyo ilikuwa Jamhuri baada ya kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Uingereza baada ya mapigano ya muda mrefu kati ya wapiganaji wa uhuru Mau Mau na wakoloni hao.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo inajivunia maendeleo makubwa ya miundo mbinu na ya kiuchumi na kuendelea kuwa nchi bora Afrika Mashariki lakini hata hivyo, suala la ufisadi na siasa za kikabila bado ni changamoto baada y miaka 53 baada ya Uhuru. Rais Uhuru Kenyatta ataadhimisha sherehe za leo jijini Nairobi.

Hayo yakijiri polisi nchini Kenya wanachunguza chanzo cha ajali iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika barabara kuu ya mji wa Naivasha kwenda Nakuru, baada ya watu 40 kupoteza maisha baada ya Lori iliyokuwa inaelekea nchini Uganda kugonga magari 13 na kuteketea moto.

Itafahamnika kwamba miili ya waliofariki imesafirishwa mjini Nairobi katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Chiromo kwa ajili ya kuitambua. polisi 11 wa kitengo cha GSU ambao humlinda rais ni miongoni mwa waliofariki.