Baraza la usalama la UN lakataa vikwazo dhidi ya Sudan Kusini
Imechapishwa:
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limekataa rasimu ya maazimio iliyopendekezwa na Marekani juu ya kuiwekea Sudan Kusini vikwazo vya silaha huku kukiwa na mgawanyiko juu ya kushinikiza viongozi wa taifa hilo kumaliza vita.
Hatua hizo zilizopendekezwa na Marekani zilipata kura saba pekee katika baraza lenye wajumbe 15 wakati mataifa 8 ikiwemo Urusi China na Japan wakikosa kupiga kura.
Kura 9 bila kura ya veto zilitakiwa ili maazimio hayo kupitishwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Marekani ikiungwa mkono na Uingereza na Ufaransa ilitetea azimio lao kuwa kuziba mianya ya silaha kuingia nchini humo ilikuwa hatua muhimu kufuatia umoja wa mataifa kuonya juu ya hatari ya kutokea mauaji ya halaiki.
Lakini Urusi, China, Japan, Malaysia,Venezuela na nyingine muhimu zaidi kutoka bara Afrika Angola, Misri na Senegal hazikupiga kura.