Habari RFI-Ki

Mswada tata wa wa mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi

Sauti 15:34
Bunge la kenya
Bunge la kenya

Spika wa Baraza la Senate nchini Kenya Ekwe Ethuro, ameagiza mswada tata wa mabadiliko ya sheria ya Uchaguzi ujadiliwe katika Kamati ya Baraza hilo ya sheria na Haki za Binadamu.Hatua hii imetuliza joto la kisiasa nchini humo na imekuja baada ya Maseneta kukutana kwa dharura hapo jana kujadili mabadiliko hayo, ambayo sasa Spika huyo ametaka wananchi kuhusishwa kikamilifu kabla ya mswada huo kurejeshwa kwenye Baraza hilo tarehe 4 mwezi Januari.