Wafungwa wa Gereza la 1930 nchini Rwanda walalamika kuhusu nyaraka za kesi zao
Imechapishwa:
Wafungwa katika gereza kuu la Nyarugenge jijini Kigali nchini Rwanda, wameingiliwa na hofu kuhusu kesi zao kuendelea, baada ya nyaraka zao muhimu kupotea baada ya Gereza hilo kuteketea kwa moto mwishoni mwa juma lililopita.
Gereza hilo linalojulikana kwa jina la 1930 liliteketea kwa moto, Jumapili jioni Desemba 25. Miongoni mwa vitu vilivyo teketezwa na moto ni pamoja na nguo za wafungwa wapatao 171 vitu vyao vya kulalia vifaa vya usafi lakini pia kinachowaumiza sana ni nyaraka za kesi zao ambazo bado zipo mahakamani.
Kwa upande wa mkurugenzi mkuu wa magereza nchini Rwanda, George Rwigamaba, ametangaza kwamba tatizo hilo litatatuliwa hrlaka iwezekanvyo ,na kila mfungwa atakaye hitaji nyaraka za kesi yake zitapatikaa kwa wepesi kwani mahakama imehizifadhi .
Hata hivyo Mamlaka ya magereza inasema kuwa inashughulikia swala zima la kuhamishaw kwa wafungwa hao na kupelekwa katika gereza nyingine mpya ya Mageragere, ingawa haikutangazwa siku maluumu ya kuhamishwa kwa wafungwa hao.