RWANDA-NJAA

Baa la njaa lakumba eneo la mashariki mwa Rwanda

Wanawake wanafanya kazi ya kilimo magharibi mwa Rwanda.
Wanawake wanafanya kazi ya kilimo magharibi mwa Rwanda. RFI/Stéphanie Aglietti

Baa la njaa katika eneo la Matimba Mashariki mwa Rwanda, limesababisha wakaazi wa eneo hilo kukimbilia nchini Uganda kwenda kutafuta chakula.

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali ngumu ya maisha inayoendelea kulikumba eneo la Matimba mashariki mwa Rwanda, idadi ya wakazi wa eneo hilo wanaokimbilia nchini Uganda kutafuta maisha inazidi kuongezeka kila uchao.

Miezi michache iliyopita serikali ya Rwanda ilitambua kwamba hali ya chakula katika baadhi ya maeneo, hasa katika mkoa wa Mashariki, inatia wasiwasi na hatua zilichukuliwa ili kuboresha hali ya mambo.

Toka wakati huo mvua zilipatikana kwa wingi na athari ya ukame na uhaba wa maji kwa mifugo na mazao vilipungua.

Lakini baadhi ya vyombo vya habari bado vinabaini kwamba kitisho cha baa la njaa badi kinashuhudiwa katika eneo la mashariki mwa Rwanda.

Baadhi ya waandishi wa habari walitembelea wilaya ya Kayonza na walishuhudia wakaazi wa wilaya hito wakikabiliwa na ukame na njaa. Miezi sita iliyopita nchi hiyo ilikabilia na kitisho cha baa la njaa na baadhi ya raia walikimbili katika nchi jirani za Uganda na Tanzania.