SUDAN KUSINI-USALAMA

Mawakili kadhaa waikimbia nchi ya Sudan Kusini kwa kuhufia usalama wao

Mkimbizi akiandamana na askari wa kulinda amani, karibu na kambi ya kulinda raia (POC) ya Umoja wa Mataifa mjini Juba, Oktoba 4, 2016.
Mkimbizi akiandamana na askari wa kulinda amani, karibu na kambi ya kulinda raia (POC) ya Umoja wa Mataifa mjini Juba, Oktoba 4, 2016. ALBERT GONZALEZ FARRAN / AFP

Zaidi ya mawakili kumi wametoroka Sudan Kusini baada ya kuhofia kuuawa. Kutoroka kwa mawakili hao kunakuja wakati hali ya usalama inazidi kuzorota katika nchi hiyo changa barani Afrika.

Matangazo ya kibiashara

Huyu hapa mwandishi wetu wa maswala ya Sudan Kusini, James Shimanyula kutupasha zaidi.

Kufikia Ijumaa hii Desemba 30, zaidi ya mawakili kumi mashuhuri wa Sudan Kusini, wametoroka nchini humo na kukimbilia katika nchi jirani za Ethiopia, Uganda, Jamhuri ya Congo na Kenya baada ya kuonywa kuwa wangeuawa na makachero wa serikali ikiwa wataendelea kuwatetea watu wanaoipinga serikali ya rais Salva Kiir.

Hali ya usalama nchini Sudan Kusini imeendelea kutisha tabgu kutokea kwa mapigano hivi karibuni kati ya jeshi linalomuunga mkono rais Salva Kiir na wapiganaji wa Riek Machar