UGANDA-MAZUNGUMZO-SIASA

Besigye atoa masharti ya kushiriki mazungumzo ya kisiasa nchini Uganda

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye.
Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye. © AFP PHOTO / ISAAC KASAMANI

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ametoa masharti matano ya kushiriki katika mazungumzo ya kisiasa nchini humo katika siku zijazo ikiwa yatafanyika.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya Uchaguzi wa mwaka uliopita, ambayo rais Yoweri Museveni alitangazwa mshindi lakini Beisgye akadai kura ziliibiwa, Baraza la Wazee nchini humo limekuwa likipendekeza kufanyika kwa mazungumzo hayo.

Beisgye ambaye amesema yuko tayari kwa mazungumzo hayo ikiwa yatakuwepo, anasisitiza kuwa msuluhishi lazima awe ni raia wa kigeni.

Wakati huo huo, kiongozi huyo wa upinzani ametangaza kile alichokita vuguvugu la serikali ya wananchi, analosema litasaidia kuwaelewesha wananchi wa taifa hilo harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini humo.