KENYA-ELIMU

Mwaka mpya wa masomo waanza Kenya

Moja ya shule katika kijiji cha Kogelo nchini Kenya, lililopewa jina laya rais wa Marekani Barack Obama.
Moja ya shule katika kijiji cha Kogelo nchini Kenya, lililopewa jina laya rais wa Marekani Barack Obama. RFI/Nicolas Champeaux

Mwaka mpya wa masomo umeanza leo nchini Kenya, baada ya kumalizika kwa muda wa mapumziko. Maelfu ya wanafunzi leo wamejiunga na masomo ya darasa la kwanza nchini Kenya, katika siku ambayo wazazi na wanafunzi wamekuwa na shughuli nyingi.

Matangazo ya kibiashara

Katika jiji kuu la Nairobi, wanafunzi wengi walikosa usafiri wa mapema kwenda kufika kutokana na wingi wa watu na uchache wa magari katika siku hii ya kwanza ya kufungua shule.

Hii ndio mara ya kwanza wanafunzi kufungua shule katika wiki ya kwanza ya mwezi Januari, baada ya Waziri wa Elimu Fred Matiangi kuanza kutekeleza mageuzi katika sekta ya elimu nchini humo.

Kwa mara ya kwanza nchini Kenya, matokeo ya taifa ya shuel ya msingi ya darasa la nane na yale ya sekondari ya kidato cha nne, yalitolewa mwaka uliopita, na kushuhudia wanafunzi wengi wakipata alama za chini.

Nchini Tanzania, wanafunzi wanatarajiwa kurejea shuleni kuanzia tarehe 9 mwezi huu.

Serikali nchini humo imekuwa ikihimiza kujengwa kwa madarasa zaidi na wanafunzi wengi kujiunga na shule za sekondari.

Nchini Uganda, wanafunzi bado wanapumzika, na watafungua shule tarehe 6 mwezi Februari.

Hata hivyo, baada ya kufungwa kwa Chuo Kikuu cha Makerere kwa muda wa miezi miwili kutokana na mgomo wa Wahahdiiri, kimefunguliwa wiki hii.

Huko Rwanda, wanafunzi watarejea madarasani, tarehe 23 mwezi huu, huku wanafunzi kutoka Burundi na DRC wakiendelea wakitarajiwa kuendelea na masomo, wakisubiri muhula mpya wa masomo mwezi Septemba.