UGANDA-AJALI

Watu 14 waangamia katika ajali ya barabarani mjini Kampala

Watu 14 wamepoteza maisha jijini Kampala nchini Uganda, baada ya kutokea kwa ajali ya barabara iliyojumuisha magari matatu. Idadi kubwa ya watu walipoteza maisha walikuwa ndani ya basi ndogo ya abiria maarufu kama Taxi nchini Uganda.

Jiji la Kampala, nchini Uganda ambapo watu 14 waliangamiaka katika ajali ya magari matatu kugongana..
Jiji la Kampala, nchini Uganda ambapo watu 14 waliangamiaka katika ajali ya magari matatu kugongana.. ©Thomas Trutschel/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya gari hilo la abiria kugongana uso kwa uso na Lori aina ya FUSO katika barabara kuu ya kutoka Mbarara kwenda Masaka.

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema, derava wa gari hilo la abiria alikuwa anakwepa kumgonga ng'ombe na kwa bahati mbaya kugongana na Lori hilo.

Mwanahabari wa kituo cha Karo FM Dennis Nahoora ni miongoni mwa watu walipoteza maisha katika jali hiyo mbaya.

Ajali hii imekuja wiki moja baada ya kutokea kwa ajali ya mashua katika Ziwa Albert na Ziwa Victoria na kusababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha.