UGANDA-SAISA-ICC

Yoweri Museveni ashitakiwa ICC

Rais Yoweri Kaguta Museveni ashtumiwa na wabunge wa upinzani kuhusika katika mauaji wakati wa vikosi vya usalama vilipovamia kasri la mfalme wa Rwenzururu, Wesley Mumbere .
Rais Yoweri Kaguta Museveni ashtumiwa na wabunge wa upinzani kuhusika katika mauaji wakati wa vikosi vya usalama vilipovamia kasri la mfalme wa Rwenzururu, Wesley Mumbere . REUTERS/James Akena

Wabunge wanne wa chama cha upinzani nchini Uganda cha FDC (Forum for Democratic Change) kutoka maeneo ya magharibi mwa Uganda, wamemshtaki kiongozi wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni, katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), iliyoko mjini Hague nchini Uholanzi.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge hao kutoka katika eneo la Kasese wanamtuhumu rais Museveni kuhusika kwa kile wamechokitaja kama mauaji mabaya wakati vikosi vya usalama vilipovamia kasri la mfalme wa Rwenzururu, Wesley Mumbere.

Wabunge hao chini ya kiongozi wa upinzani bungeni na mbunge wa FDC wa Kasese Winnie Kizza, wameyasema hayo Jumanne hii mjini Kampala, walipokuwa katika mkutano na waandishi wa habari.

Wakati huo huo kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye ametoa masharti matano ya kushiriki katika mazungumzo ya kisiasa nchini humo katika siku zijazo ikiwa yatafanyika.

Baada ya Uchaguzi wa mwaka uliopita, ambayo rais Yoweri Museveni alitangazwa mshindi lakini Beisgye akadai kura ziliibiwa, Baraza la Wazee nchini humo limekuwa likipendekeza kufanyika kwa mazungumzo hayo.

Beisgye ambaye amesema yuko tayari kwa mazungumzo hayo ikiwa yatakuwepo, anasisitiza kuwa msuluhishi lazima awe ni raia wa kigeni.

Bw Besigye ametangaza kile alichokita vuguvugu la serikali ya wananchi, analosema litasaidia kuwaelewesha wananchi wa taifa hilo harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini humo.