KENYA-AJALI

Watu 11 wapoteza maisha katika ajali ya barabarani Kisumu

Ajali za barabarani zimekithiri, Watu 11 wapoteza maisha katika ajali ya barabarani Kisumu, nchini Kenya.
Ajali za barabarani zimekithiri, Watu 11 wapoteza maisha katika ajali ya barabarani Kisumu, nchini Kenya. EMMANUEL AREWA / AFP

Watu 11 wamepoteza baada ya kutokea kwa ajali ya barabara katika Kaunti ya Kisumu Magharibi mwa Kenya. Ajali za barabarni zimekithiri katika nchi za Afrika hasa afrika ya Mashariki

Matangazo ya kibiashara

Kamishena wa Kaunti ya Kisumu, Mohammed Maalim amesema chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni mwendo wa kasi wa gari la abiria maarufu kama Matatu ambalo pia lilikuwa limejaa kupita kiasi.

Ripoti zinasema kuwa, gari hilo la abiria lilikuwa linatoka katika mji wa Sirare karibu na mpaka wa Tanzania kwenda mjini Kisumu likiwa na idadi kubwa ya abiria.

Inaarifiwa kuwa gari hilo liliondoka barabarani na kuanguka shimoni katika eneo la Nyakatch, asubuhi ya leo.

Serikali ya Kaunti hiyo inasema inachunguza ni kwanini gari hilo lilikuwa na abiria wengi.

Ajali nyingine kama hii ilitokea jijini Kampala nchini Uganda Jumatano wiki hii na kusababisha vifo vya watu 14.