RWANDA-KIGELI-UFALME

Mwili wa mfalme Kigeli wawasili Rwanda

Kigeli V, mfalme wa mwisho wa Rwanda,ambaye alifariki dunia akiwa uhamishoni mjini Washingtonakiwa na umri wa miaka 80 .
Kigeli V, mfalme wa mwisho wa Rwanda,ambaye alifariki dunia akiwa uhamishoni mjini Washingtonakiwa na umri wa miaka 80 . Rwanda Library/CC/Wikimedia Commons

Mwili wa mfalme wa mwisho nchini Rwanda, Kigeli wa 5umewasili Jumatatu hii mjini Kigali, nchini Rwanda baada ya kesi ya mahakama kati ya familia yake, kuhusu ni wapi angezikwa.

Matangazo ya kibiashara

Kifo cha mfalme Kigeli kilizua mzozo ndani ya familia, kati ya ile inayoishi nchini Marekani na iliyo nchini Rwanda kuhusu ni wapi angezikwa kabla ya mahakama ya Marekani kutoa hukumu kuwa atazikwa nyumbani kwao.

Picha ya Kigeli wa 5,  mfalme wa Rwanda kuanzia mwaka 1959 hadi mwaka 1961.
Picha ya Kigeli wa 5, mfalme wa Rwanda kuanzia mwaka 1959 hadi mwaka 1961. Getty images/Universal History Archive/UIG

Mfalme Kigeli alikuwa akiishi uhamishoni mjini Washington, nchini Marekani tangu mwaka 1992, na aliaga dunia Oktoba 16 akiwa na umri wa miaka 80.

Hata hivyo baraza la kifalme la mfalme Kigeli lilisema kwenye taarifa kuwa hakutaka kuzikwa nchini Rwanda ikiwa serikali ya sasa ambayo ilipinga ufalme wake ilikuwa bado mamlakani.

Mfalme wa mwisho wa Rwanda, Kigeli wa 5, aliyetimuliwa madarakani tangu miaka hamisini iliyopita, aliishi uhamishoni nchini Marekani tangu mwaka 1992.

Jean-Baptiste Ndahindurwa ni jina lake la ubatizo, alikua na umri wa miaka 23 wakati alikabidhiwa kiti cha enzi mwaka 1959. Wakati huo, Rwanda ilikua chini ya usimamizi wa Ubelgiji, na Mwami, mfalme wa Rwanda, hakua na hadhi yoyote kama watangulizi wake.

Mwaka 1961, Ubelgiji ilianzisha mchakato wa uhuru wa ndani na kura ya maoni ilipigwa. 80% ya Wanyarwanda walipiga kura ya kufuta utawala wa kifalme. Kigeli V, ambaye tangu wakati huo aliishi uhamishoni, hakuhudhuria shereshe za uhuru wa Rwanda, uliotangazwa mwezi Julai 1962.

Mfalme Kigeli wa 5 alihamia nchini Marekani tangu mwaka 1992, baada ya kuishi miaka kadhaa nchini Tanzania, Uganda na Kenya. mwandishi wa habari wa Marekani ambaye ni wa mwisho kukutana naye akiwa ukimbizini anasema mfalme huyo alikua akiishi kwa shida katika kitongoji kimoja mjini Washington kwa misaada ya kijamii ya Marekani na michango kutoka wa raia wa Rwanda waishio ugenini.

Akiwa uhamishoni kwa zaidi ya miaka hamsini, na licha ya wito uliyotolewa na chama cha Green Party nchini Rwanda, Kigeli wa 5 hakupata nafasi ya kuiona tena nchi yake, ambapo alitawala muda mfupi.