Watu 40 wapoteza maisha katika ajali ya boti nchini Tanzania

Manusura wabeba maiti ya abiria baada ya kuzama kwa chombo cha kuvusha watu katika bandari ya Zanzibar Julai 19, 2012. Ajali za kuzama kwa mashua na boti hua zikitokea mara kwa mara nchini Tanzania.
Manusura wabeba maiti ya abiria baada ya kuzama kwa chombo cha kuvusha watu katika bandari ya Zanzibar Julai 19, 2012. Ajali za kuzama kwa mashua na boti hua zikitokea mara kwa mara nchini Tanzania. REUTERS/Thomas Mukoya

Watu arobaini walipoteza maisha katika ajali ya boti ambayo ilizama kaskazini mashariki mwa Tanzania. Boti ambayo iliku aikitokea katika bandari ya tanga ikielekea katika visiwa vya Pemba.

Matangazo ya kibiashara

Boti hiyo ilikua imebeba watu 50 wakati ilipozama usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne hii Januari 10.

Miili kumi na mbili imepatikana na watu tisa waliokolewa, polisi imesema.

Boti hilo lilikua likielekea katika visiwa vya Pemba ikitokea katika bandari ya Tanga.
Sababu za ajali hiyo hazijajulikana kwa mujibu wa polisi.