BURUNDI

Mazungumzo kuhusu Burundi kufanyika Arusha juma lijalo

Mwezeshaji wa usuluhishi wa mgogoro wa Burundi, Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa mwanzoni mwa juma lijalo anatarajiwa kuendesha mkutano kwa ajili ya kutathimini hatua iliyofikiwa katika usuluhishi wa mgogoro huo.

Mwezeshaji wa mgogoro wa Burundi Benjamin William Mkapa, rais mstaafu wa Tanzania
Mwezeshaji wa mgogoro wa Burundi Benjamin William Mkapa, rais mstaafu wa Tanzania rfikiswahili/Ali Bilal
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo utafanyika jijini Arusha nchini Tanzania na unalenga kuwakutanisha wanasiasa walioko nje ya nchi hiyo ambao hawakupata fursa kushiriki katika mazungumzo ya amani ya awali.

Katika mkutano huo Mkapa atatoa mwenenendo wa mazungumzo ya amani ya Burundi na kuweka bayana changamoto anazokabiliana nazo pamoja na hatua za kuchukua ili mazungumzo hayo yaendelee.

Burundi ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwania muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo mwaka 2015