BURUNDI-MAZUNGUMZO

Mazungumzo kuhusu Burundi kufanyika Jumatatu

Mazungumzo baina ya Wurundi yazinduliwa rasmi nchini Uganda Jumatatu, Desemba 28, kupitia upatanishi wa rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni.
Mazungumzo baina ya Wurundi yazinduliwa rasmi nchini Uganda Jumatatu, Desemba 28, kupitia upatanishi wa rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni. RFI-KISWAHILI

Mratibu wa mazungumzo ya Warundi, Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa anatarajiwa kukutana Jumatatu Januari 16, 2017 na upinzani wa utawala wa Pierre Nkurunziza ulio uhamishoni, ikiwa ni mwendelezo wa mazungumzo ya kusaka amani ya kudumu yanayoendelea nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo baadhi ya wanasiasa wa muungano wa upinzani ulio uhamishoni CNARED wamekataa katu katu kushiriki katika mazungumzo hayo, wakibaini kwamba Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa anaegemea upande wa serikali baada ya kuonyesha msimamo katika ziara alioifanya mwaka jana mjini Bujumbura.

CNARED inasema wakati huo, Benjamin Mkapa alisema kuwa anamtambua Pierre Nkurunzia kama rais halali wa Burundi ambaye alichaguliwa na wananchi, huku akibaini kuwa wale wanaopinga ni Wendawazimu, imesema CNARED.

CNARED inasema rais mtaafu Benjamin Mkapa alisikika akisema kuwa atawasaidia Warundi kuandaa uchaguzi wa mwaka 2020, wala haoni tatizo jingine.
Wakati huo huo baadhi ya wanasiasa wa muungano huo wametangaza kwamba watashirii katika mazungumzo hayo ya Jumatatu Januari 16. Si mara ya kwanza kujitokeza mgawanyiko katika muungano wa huo CNARED.

Katika mkutano huo Mkapa atatoa mwenenendo wa mazungumzo ya amani ya Burundi na kuweka bayana changamoto anazokabiliana nazo pamoja na hatua za kuchukua ili mazungumzo hayo yaendelee.
Burundi ilitumbukia katika mgogoro wa kisiasa wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwania muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo mwaka 2015.

Machafuko nchini Burundi yamesababidha watu zaidi ya 600 kupoteza maisha kwa mujibu wa mashirika ya kimataifa ya haki za Binadamu ( Amnesty International na Human Right Watch), huku watu zaidi ya laki tatu wakilazimika kuyahama makazi yao.

Hata hivyo visa vya mauaji na utekaji nyara vinaendelea kushuhudiwa hapa na pale nchini Burundi.