TWANDA-ICT-MAENDELEO

Unesco: Rwanda imepata mafanikio makubwa katika maendeleo ya Intaneti

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) limeitaja Rwanda kama moja ya mifano ya mafanikio ya maendeleo katika Intaneti barani Afrika. Rwanda kwa sasa ni moja ya nchi zinazoongoza katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) barani Afrika.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame aelezea mafanikio yaliyofikiwa na nchi yake katika sekta ya Intaneti kupitia ushirikiano wa sekta binafsi kama mshirika katika uvumbuzi na sera ya uwekezaji ya maendeleo ya kidijitali nchini Rwanda.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame aelezea mafanikio yaliyofikiwa na nchi yake katika sekta ya Intaneti kupitia ushirikiano wa sekta binafsi kama mshirika katika uvumbuzi na sera ya uwekezaji ya maendeleo ya kidijitali nchini Rwanda. REUTERS/Ruben Sprich
Matangazo ya kibiashara

Katika Kongamano la Kiuchumi Duniani lililofanyika mjini Davos, nchini Uswisi, kuanzia Januari 17 hadi 20, 2017, Irina Bokova, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu Sayansi na Utamaduni (Unesco) aliitaja Rwanda kama moja ya mifano ya mafanikio katika maendeleo ya intaneti duniani, kwa mujibu wa RFI na Shirika la Habari la Ecofin. Kiongozi huyo alitolea wito nchi nyingi ambazo bado zina kiwango cha chini kwa matumizi ya Intaneti kuiga mfano wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki kwa kuungana na kuboresha mazingira ya maisha ya watu bilioni 3.9 ambao bado hawafajafikia hatua hii.

Irina Bokova alikuwa akiongea katika kikao maalum cha Tume kuhusu masafa marefu kwa ajili ya Maendeleo Endelevu, kiliyoandaliwa na Muungano wa Kimataifa kwa ajili ya Mawasiliano, kikao ambacho kilifanyika tarehe 17 Januari 2017. Katika kikao hicho, Rais wa Rwanda Paul Kagame, mmoja wa viongozi wa Tume hiyo, alielezea mafanikio yaliyofikiwa na nchi yake katika sekta ya Intaneti kupitia ushirikiano wa sekta binafsi kama mshirika katika uvumbuzi na sera ya uwekezaji ya maendeleo ya kidijitali nchini Rwanda. Kampuni ya Korea Telecom Networks Rwanda (KTRN), inayotoa huduma ya Intaneti kwa kiwango kikubwa na kwa bei nafuu, na ambayo kwa sasa imeanza kusambaza mitambo yake nchi nzima, imechangia pakubwa katika sekta hiyo.

Katika kata kunakofanyika shughuli za biashara mjini Kigali.
Katika kata kunakofanyika shughuli za biashara mjini Kigali. RFI/Stéphanie Aglietti

"Ushirikiano wa sekta ya umma na ile ya kibinafsi ni muhimu kwa maendeleo ya teknolojia ya kidijitali, kwa kuzingatia kwamba kutoa huduma ya Intaneti katika maeneo ambapo haipo, inaleta maendeleo makubwa. Kutoa huduma ya Intaneti kwa idadi hii kubwa [ya watu] inachangia mapato. Kama washirika, tuna nafasi ya kutafakari kazi inayovutia bila kujali gharama kubwa ambayo ingeweza kuzorotesha upatikanaji wa huduma hiyo, "alisema Rais Kagame. Alibaini kwamba Rwanda imefikia 30% kwa kutoa huduma ya Intaneti kati ya mwaka 2003 na 2016 kutokana na kushiriki kwa sekta binafsi katika mkakati na mipango ya kitaifa ya maendeleo ya kiteknolojia.

Itafahamika kwamba washirika wakubwa wa KTRN ni Tigo, MTN, Airtel, ISCO, Popconn, ISPA, Tnsp, G-MAX,...

Watumiaji wengi wa Intaneti barani Afrika hutumia simu ya mkononi.
Watumiaji wengi wa Intaneti barani Afrika hutumia simu ya mkononi. Photographer: Nadine Hutton/Bloomberg via Getty Images

Mwezi Januari mwaka huu Waziri wa Vijana na Teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT), alisema Rwanda inalenga kutoa huduma ya 92% ya mtandao wa masafa marefu wa (4G) wenye kasi kubwa mwaka huu.

Jean Philbert Nsengimana, Waziri wa Vijana na Teknolojia wa Habari na Mawasiliano (ICT), aliwaambia waandishi wa habari kwamba nchi hiyo inataka mtandao wa 4G usambazwe katika maeneo ya vijijini, kinyume na kile kinachofanyika leo mjini Kigali.

"tunataka kila Mnyarwanda apate huduma ya Intaneti yenye kasi na yenye kuaminika kwa shughuli zake za kibiasharana shughuli nyingine zinazohitaji Intaneti," Bw Nsengimana alisema.