Rais wa Uturuki awasili Tanzania
Imechapishwa: Imehaririwa:
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amewasili nchini Tanzania jioni ya siku ya Jumapili kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Rais Erdogan ambaye ameambatana na Mkewe, ameongoza ujumbe wa watu 150 wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Maafisa kutoka Serikalini na Wafanyabiashara kutoka Uturuki.
Lengo la ziara hiyo ni kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Uturuki na Tanzania pamoja na kupanua fursa za uwekezaji hususan katika maeneo ya biashara na uwekezaji ambapo baada ya kuwasili atakutana na Rais Magufuli na baadaye Marais hao watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali.
Uhusiano kati ya Tanzania na Uturuki uliimarika zaidi mwaka 2009 mwezi Mei baada ya kufunguliwa kwa mara nyingine kwa Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzani.