TANZANIA-UTURUKI-USHIRIKIANO

Tanzania na Uturuki zatiliana saini mikataba 9 ya ushirikiano

Uturuki na Tanzania zimetiliana saini mikataba 9 ya ushirikiano katika sekta mbalimbali. Rais wa Uturuki Recep tayyip Erdogan aliwasili Jumapili Januari 22 mjini Dar es Salaam, nchini Tanzania, na ataendelea na ziara hiyo katika mataifa kadhaa barani Afrika.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, aendelea na ziara yake barani Afrika.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, aendelea na ziara yake barani Afrika. REUTERS/Umit Bektas
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya ziara ya siku mbili ya rais wa Uturuki Tayyip Recep Erdogan ambaye anazuru bara la Afrika, na atazuru Madagascar na Jumatatu wiki hii amekwenda Msumbiji.

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema, mikataba hii itadumisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili.

Naye rais Erdogan ameitaka Tanzania na mataifa mengine ya Afrika, kusaidia nchi yake kukabiliana na makundi ya magaidi na watu wanaopanga kuiangusha serikali yake kama ilivyokuwa mwaka uliopita.