Kenya yamzuia Mwanaharakati anayetafutwa nchini Sudan Kusini
Imechapishwa: Imehaririwa:
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch linasema mwanaharakati maaurufu kitoka nchini Sudan Kusini Dong Samuel Luak, anazuiliwa jijini Nairobi nchini Kenya na huenda akarudishwa kwa nguvu nchini mwake.
Luak ambaye pia ni wakili, amekuwa akipokea vitisho vya kuawa na kuna uwezekano mkubwa akakamtwa pindi tu atakaporejeshwa nchini mwake.
Human Rights Watch, inasema wakili huyo alikimbilia nchini Kenya mwaka 2013 baada ya kupata vitisho vya kuuawa kutoka kwa serikali ya Juba, baada ya kumtetea mwanasiasa mmoja nchini humo dhidi ya tuhma za uhaini, lakini pia katika harakati za kushtumu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo.
Ripoti kutoka Shirika hili linasema kuwa Luak amenyimwa haki ya kumwona wakili wake.
Kenya haijazungumzia ripoti hii ya HRW.
Mwaka uliopita, msemaji wa kiongozi wa waasi Riek Machar ambaye kwa sasa anaishi nchini Afrika Kusini James Gatdet Dak, alikamatwa na kurudishwa kwa nguvu nchini Sudan Kusini na kukamatwa alipofika jijini Juba.