TANZANIA-UKIMBIZI

Tanzania yajaribu kuzuia kuingia kwa wakimbizi kutoka nchi jirani

Wakimbizi wa Burundi wakielekea katika kambi ya Nduta mkoani Kigoma, mwezi Oktoba 2015.
Wakimbizi wa Burundi wakielekea katika kambi ya Nduta mkoani Kigoma, mwezi Oktoba 2015. AFP Photo/Oxfam/Mary Mndeme

Serikali ya Tanzania imetangaza kuwa hairuhusu tena hadhi ya ukimbizi kwa makundi ya wakimbizi kutoka nchi jirani. Sababu iliyotolewa: ni kuingia sambamba ya idadi kubwa ya silaha kinyume cha sheria. Serikali ya Tanzania imesema wakimbizi tu wanaweza kufanya maombi ya ulinzi, lakini kila mmoja kwa jina lake.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Tanzania, kupitia Waziri wake wa Mambo ya Ndani pia imebaini kwamba wakimbizi kutoka eneo la Maziwa Makuu wanaingia nchini Tanzania kwa sababu za kiuchumi na si kwa sababu za ghasia za kikabila na kisiasa.

Jumatano iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania, Mathias Chikawe alizuru mkoa Kigoma, ambao inawapa hifadhi idadi kubwa ya wakimbizi ambao walikimbia gmachafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi.

Zaidi ya silaha 5,000 za kivita zilizopokonywa makundi ya wakimbizi kutoka nchi jirani zilichomwa moto.

Katika hotuba yake, Waziri wa Mambo ya Ndani amebainisha kwamba kumekua na wakimbizi wengi, biashara ya silaha, na kuongezeka kwa uhalifu.

Wakati huo huo, Mwigulu Nchemba ametangaza kwamba anauta utoaji wa hadhi ya ukimbizi kwa makundi yaliyoorodheshwa, huku akibaini kwamba ombi la kila mkimbizi kuhusu ulinzi wake litajadiliwa.

Waziri Mathias Chikawe alisema serikali ya Tanzania inaona kwamba hakuna ukosefu wa usalama katika nchi jirani. Na kama watu wanakimbia nchi zao ni kwa sababu za kiuchumi, aliongeza Bw Chikawe.

Wadadisi wanasema huenda serikali ya Tanzania imekana kuwepo na hali mbaya ya usalama katika nchi za maziwa Makuu, hususan Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kukataa kuhatarisha uhusiano wa kidiplomasia na viongozi wa nchi hizo jirani.

Pamoja na wakimbizi 300 000 waliotawanywa katika makambi manne, Tanzania bado ni nchi ambayo ina wakimbizi wengi kutoka nchi jirani kwa kipindi cha miaka thelathini sasa.