Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI

Rais Kiir asema atawania urais mwaka 2018

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Stringer
Ujumbe kutoka: Victor Melkizedeck Abuso
1 Dakika

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametangaza kuwa atawania urais baada ya kumalizika kwa muda wa serikali ya mpito mwaka ujao.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza akiwa katika jimbo la Yei, rais Kiir alisisitiza kuwa ni lazima raia wa nchi hiyo wapige kura mwaka 2018.

Kiir amesema kuwa uchaguzi huo utaamua mustakabali wa taifa hilo ambalo lilipata uhuru mwaka 2011 baada ya kutengana na Sudan.

Kiongozi huyo amemtaka kiongozi wa waasi Riek Machar anayeishi nchini Afrika Kusini kuanza maandalizi ya kushiriki katika Uchaguzi huo na kurejea nyumbani ili kushiriki katika Uchaguzi huo.

Aidha, amemtaka Machar kuyaambia makundi ya waasi yanayopigana nchini humo na yale yanayoishi nje ya nchi kurejea nyumbani ili kushiriki katika uchaguzi huo wa kidemokrasia.

Kiir na Machar walitia saini mkataba wa amani kumaliza vita nchini mwao mwaka 2015 jijini Addis Ababa lakini wakashindwa kuutekeleza.

Mwezi Julai mwaka 2016, kulitokea na mapigano makali jijini Juba na kusababisha Machar na wafuasi wake kukimbia nchi hiyo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.