Habari RFI-Ki

Raia kutoka maziwa makuu wanazungumziaje hatua ya Tanzania kupiga marufuku pombe za viroba

Sauti 10:01
Shehena ya pombe aina ya viroba ambavyo vimekatazwa rasmi kutumika Tanzania.
Shehena ya pombe aina ya viroba ambavyo vimekatazwa rasmi kutumika Tanzania. Issa Michuzi/Blog

Makala ya Habari Rafiki hii leo inazungumzia uamuzi wa Serikali ya Tanzania kupiga marufuku matumizi ya pombe aina Viroba, amri ambayo imeanza kutekelezwa Machi Mosi mwaka hu, hivi sasa mtu atakayekamatwa anatengeneza ama kunywa pombe za kwenye vifungashio, atachukuliwa hatua na hata kwenda jela. Wasikilizaji wa Afrika Mashariki na Kati na dunia kwa Ujumla wanazungumziaje uamuzi huu? Ungana na mtangazaji wa makala haya hivi leo, Emmanuel Makundi.