TANZANIA-HAKI
Matthew Maliango ahukumia kifungo cha miaka 12 jela
Mwindaji haramu wa pembe za ndovu nchini Tanzania anayefahamika kwa jina maarufu kama Shetani amefungwa jela miaka 12.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Boniface Matthew Maliango, alikamatwa akiwa na pembe za ndovu 118 zenye thamani ya Dola 860,000 na kufunguliwa mashtaka.
Hii ni hatua kubwa katika vita dhidi ya uwindaji haramu katika taifa hilo la Afrika Mashariki, ambalo wanyamapori kama ndovu wapo hatarini kutoweka kutokana na ongezeko hili.
Hatua hii inakuja dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya kupambana na wanyamapo huku Shirika la Chakula duniani FAO likitoa wito wa wanyamapori kuhifadhiwa.