Muwindaji hatari wa wanyama pori nchini Tanzania afungwa miaka 12 jela
Imechapishwa:
Muwindaji haramu wa pembe za ndovu nchini Tanzania ambaye pia alifahamika kama shetani wa wanyama amehukumiwa kifungo cha miaka 12 jela.
Boniface Metthew Maliango alikamatwa akiwa na pembe za ndovu 118 zenye thamani ya dola za Marekani 860,000 na kufunguliw amashtaka.
Boniface Matthew Maliango, ambaye amekwepa kukamatwa mara kadha alitiwa mbaroni mwezi Oktoba.
Hii ni hatua kubwa katika vita dhidi ya uwindaji haramu katika taifa la Afrika mashariki ambalo wanyama pori kama ndovu wapo hatarini kutoweka kutokana na tatizo la uwindaji haramu.
Hatu ahii inkauja wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kuhifadhi wanyama pori shirika la chakula duniani FAO likitoa wito wa wanyama pori kuhifadhiwa.