Katibu mkuu wa UN kuzuru Kenya leo Jumapili
Imechapishwa:
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo Jumapili atazuru nchini Kenya kwa mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo kuhusu masuala ya kikanda,wakati huu nchi za Sudan Kusini na Somalia zikikabiliwa na tishio la njaa, msemaji wake amearifu.
Somalia inakabiliwa na tishio la njaa wakati maeneo ya kaskazini ya Sudan Kusini tayari yana kabiliwa na njaa.
Kenya ni nchi muhimu katika juhudi za amani nchini Somalia na imekubali kuchangia wanajeshi katika kikosi kipya cha kikanda cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.
Guterees ambaye alichunua nafasi hiyo mwezi Januari anashinikiza mkakati mpya ili kukomesha vita nchini Sudan Kusini iliyodumu kwa miaka mitatu sasa.