SUDAN KUSINI

Mdahalo wa kitaifa kuhusu amani ya Sudan Kusini watarajiwa mwishoni mwa juma hili

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Gaël Grilhot/RFI

Mdahalo wa kitaifa unatarajiwa kufanyika nchini Sudan Kusini mwishoni wa juma hili kwa lengo la kumaliza mapigano ya kikabila ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa miaka mitatu sasa

Matangazo ya kibiashara

Wito wa kufanyika kwa madahalo huu ulitolewa na rais Salva Kiir mapema mwezi uliopita ili kurejesha amani Sudan Kusini ambapo aliwaalika waasi kushiriki lakini sasa amebadili msimamo wake na kusema kuwa waasi wataruhusiwa kushiriki pale tu watakapokubali kuweka chini silaha.

Hata hivyo waasi wa Sudani Kusini kupitia kwa Meja Jenerali Nyagwal Ajak Deng, mmoja wa Mkamanda wa vikosi vya Riek Machar amesema mdahalo huo kamwe hautafua dafu na wao hawatahudhuria

Sudani kusini ilitumbukia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe takribani miaka mitatu iliyopita baada ya rais Salva Kiir kumfuta kazi aliyekuwa makamu wake Riek Machar ambaye kwa sasa anaongoza vikosi vya uasi dhidi yake na takribani ikataba saba imesaini kukomesha mapigano bila mafanikio