TANZANIA-SIASA

Chama tawala nchini Tanzania CCM chawafuta uanachama wasaliti

Mwenyekiti wa chama tawala nchini Tanzania, CCM na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa chama tawala nchini Tanzania, CCM na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. DR

Chama tawala nchini Tanzania,CCM kimewatimua baadhi ya wanachama huku wengine wakipewa onyo kali na kuvuliwa uongozi baada ya kupatikana na makosa ya kimaadili.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa waliofukuzwa uanachama ni pamoja na mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT Sophia Simba.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao kilichofanyika jumamosi Dodoma nchini Tanzania kikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho raisi John Pombe Magufuli.

Katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho Humphrey Polepole amethibitisha hatua hizo kuchukuliwa dhidi ya baadhi ya wanachama wa CCM.

Hayo yanajiri wakati duru za habari nchini Tanzania zikiarifu kuhusu Wabunge wawili na aliyekuwa naibu waziri wa fedha, Adam Malima kuhojiwa na polisi mjini dodoma kufuatia madai ya kutaka kufanya vurugu katika vikao vya CCM.