UN-SUDAN KUSINI

Mashirika ya misaada ya kimataifa yapinga nyongeza ya tozo ya viza kwa wafanyakazi wa kigeni

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir

Mashirika ya misaada ya kimataifa yamekemea uamuzi wa Sudani kusini kuongeza ada ya viza za wafanyakazi wa kigeni kufikia kiasi cha dola za marekani elfu kumi na kuonya kuwa hatua hiyo itazidisha janga la kibinadamu linalokabili nchi hiyo yenye vita.

Matangazo ya kibiashara

Muwakilishi wa shirika la Amnesty International Elizabeth Deng amesema serikali na jeshi vimechangia pakubwa katika janga la kibinadamu na sasa vinataka kujinufaisha kupitia janga hilo.

Mikakati ya serikali iliyotangazwa March 2 itaongeza ada ya wafanyakazi wa kigeni kutoka dola mia moja na mia tatu hadi kufikia dola elfu moja na elfu kumi kwa mwaka kutegemea na sifa za mfanyakazi.

Hatua hizo zitazalisha mapato katika taifa hilo ambalo mapato yake makubwa yamekuwa yakipatikana kupitia mafuta lakini mashirika ya misaada yamepinga hatua hiyo.

Hayo yanajiri wakati huu Umoja wa mataifa ukionya juu ya janga la kibinadamu linaloikabili dunia na kueleza kuwa ni wakati mgumu zaidi tangu kumalizika kwa vita ya pili ya dunia ambapo zaidi ya watu milioni 20 wanakabiliwa na njaa na ukame katika mataifa manne Sudani kuisni ikiwemo.