BURUNDI-MALARIA-AFYA

Burundi yatangaza kukumbwa na janga la malaria

Anopheles ni mbu anayehusika na  maambukizi ya malaria kwa binadamu
Anopheles ni mbu anayehusika na maambukizi ya malaria kwa binadamu James D. Gathany/wikimedia.org

Serikali ya Burundi imetangaza kuwa nchi yake imekubwa na janga la malaria na mikoa ya kaskazini mwa nchi hiyo ndio imeathirika zaidi. Tangazo hilo lilitolewa na Waziri wa Afya Josiane Nijimbere siku ya Jumatatu mchana Machi 13 wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Matangazo ya kibiashara

Karibu watu milioni mbili wameambukizwa katika kipindi cha miezi mitatu na virusi vinavyosababishwa na mbu.Mwaka 2016, watu milioni nane waliambukizwa ugonjwa huo na watu 3,000 walifariki katika nchi hii yenye wakazi wasiopungua milioni 8 .

Hii ni hali isiyokuwa ya kawaida, Shirika la Afya Duniani limesema. Kwa sababu ya ongezeko la joto duniani, upanuzi wa maeneo ya kulima zao la mchele na mgogoro wa chakula unaosababisha watu kuyahamia sehemu nyingine, malaria huathiri maeneo ambayo mpaka sasa yametelekezwa, hasa katika maeneo yenye milima mrefu.