TANZANIA-MAREKANI-VYOMBO VYA HABARI

Wanahabari tisa wa TBC 1 wasimamishwa kazi kwa kutoa habari ya uongo

Watangazaji tisa wa TBC 1 walioandaa, kuandika na kutangaza habari juu ya Rais wa Marekani Donald Trump kumsifia Rais Magufuli wamesimamishwa kazi kwa kutangaza habari ya uongo.

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imechukuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC, Ayubu Rioba ambae alisema inasemekana kuwa  habari hiyo ni ya uongo na Rais Trump hakufanya hivyo.

Waliosimamishwa kazi ni pamoja na mtangazaji aliyeisoma habari hiyo, Gabriel Zakaria na wengine ni Elizabeth Mramba, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhan Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai.

Mkurugenzi wa TBC, Dk. Ayoub Riyoba amethibitisha kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa wafanyakazi hao kufuatia kosa hilo walilolifanya.

"Kosa hili lisingetokea kama taratibu zote za uhariri ili kuthibitisha ukweli wa habari hii zingelifuatiwa," alisema Mkurugenzi wa TBC 1.

►Hii ndo taarifa ya uongo iliyosomwa TBC