BURUNDI

Mafuriko yaua sita Burundi

Wakazi wa Bujumbura, wakipita katika maji yaliyosababishwa na mafuriko ya mvua mjini humo 17 mars 2017.
Wakazi wa Bujumbura, wakipita katika maji yaliyosababishwa na mafuriko ya mvua mjini humo 17 mars 2017. AFP

Takribani watu sita wamefariki dunia nchini Burundi baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko na uharibifu mkubwa,serikali imefahamisha.

Matangazo ya kibiashara

Mvua kali iliyoambatana na upepo ilipiga mikoa kadhaa mwishoni mwa juma alithibitisha makamu wa kwanza wa raisi Gaston Sindimwo.

Katika mji wa kaskazini magharibi Mabayi,maporomoko yaliharibu nyumba kadhaa ambapo waokozi walifanikiwa kuokoa watu watano na kuarifu kuwa juhudi za uokozi zinaendelea.

Mafuriko katika jiji la bujumbura yamesababisha vifo vya watu watano.

Makamu wa kwanza wa raisi Gaston Sindimwo ameeleza kuwa hilo ni janga limeikumba nchi ambapo watu kadhaa wamejeruhiwa huku makazi 162 yamethibitika kuharibiwa.

Hata hivyo amewahakikishi araia kuwa serikali inafanya juhudi ili kutoa misaada na kushughulikia waathirika.