TANZANIA

Rais wa benki ya dunia kuzuru Tanzania

Rais wa benki ya dunia dokta Jim Yong Kim anazuru Tanzania kuanzia leo Jumapili hadi Machi 21 kwa ziara ya kikazi , imeeleza taarifa ya kitengo cha mawasiliano ya serikali, wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki

Rais wa benki ya Dunia, Jim Yong Kim
Rais wa benki ya Dunia, Jim Yong Kim UN Photo/Rick Bajornas
Matangazo ya kibiashara

Akiwa nchini Tanzania Jim Yong atafanya mazungumzo na rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kesho Jumatatu machi 20 ikulu jijini Dar es Salaam na kushiriki uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara za juu katika eneo la Ubungo.

Aidha baada ya zoezi hilo viongozi hao watashuhudia zoezi la uwekaji saini wa mikataba mitatu ya uboreshaji miundombinu ya usafiri Dar es Salaam, uboreshaji miundombinu na huduma za msingi katika baadhi ya miji.

Aidha dokta Kim atapata nafasi ya kutembelea shule ya msingi Zanaki ambayo ni moja ya shule zinazonufaika na mpango wa kuboresha ubora wa elimu ya msingi unaogharamiwa na benki ya dunia.

Ziara ya Kim inakuja kufuatia ziara iliyofanywa na makamu wa rais wa benki ya dunia kanda ya Afrika Makhtar Diop mwezi Januari mwaka huu nchini Tanzania.