RWANDA-ISRAEL

Kagame asifu uhusiano wa Rwanda na Israel, aunga mkono taifa la Wayahudi

Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame. REUTERS/Ruben Sprich

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amekuwa kiongozi wa kwanza barani Afrika kuhutubia kungmanao kubwa la watu wa Washington ambao wanaiunga mkono Serikali ya Israel, akisifu taifa hilo la Kiyahudi kuwa mfano kwa taifa lake kuzaliwa upya baada ya mauaji ya kimbari.

Matangazo ya kibiashara

Rais Kagame alikuwa kiongozi wa waasi aliyezima na kumaliza mauaji ya Rwanda ya mwaka 1994 kati ya Wahutu na Watutsi, ambapo ameliongoza taifa hilo toka mwaka 2000, wakati huu taifa lake likipona majeraha ya mauaji hayo na kuwa taifa la mfano kwenye ukanda wa nchi za Afrika Mashariki.

Rais Kagame amehudhuria mkutano wa mwaka kuhusu Israel na Marekani, ambapo amelisifu taifa hilo baada ya kufanikiwa kujiimarisha hata baada ya mauaji ya Holocaust na kuahidi Rwanda kuiunga mkono.

“Usalama wa raia ambao awali walilengwa kwa mashambulizi ili watokomee kamwe hauwezi kuwa wa kimwili tu,” alisema rais Kagame ambaye alishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria kongamano hilo.

“Hadi pale aidiolojia za kujaribu kueleza mauaji haya kama etu ni uzalendo zitakaposhindwa, dunia yetu bado sio salama, sio kwetu na sio kwa yeyote yule.” alisema rais Kagame.

Kauli ya Kagame inaonekana kama muendelezo wa kurejea kwa uhusiano wa kawaida kati ya Israel na nchi za Afrika, ambapo awali uhusiano huu haukuwa katika hali ya kawaida.

Nchi nyingi za Afrika zilikuwa zinaiona Israel kama muungaji mkono wa utawala wa kibaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, lakini katika miaka ya hivi karibuni Israel imeanza kurejesha uhusiano wa kawaida wa Kidiplomasia.