KENYA-SIASA

Upinzani nchini Kenya wasema utakuwa na kituo cha kujumuisha matokeo ya urais

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya NASA, umetangaza kuwa utakuwa na kituo chake cha kujumuisha matokeo ya uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Wanasiasa wa upinzani Kalonzo Musyoka kushoto na Raila Odinga kulia, Machi 25 wakiwa katika mkutano wa kisiasa jijini Nairobi
Wanasiasa wa upinzani Kalonzo Musyoka kushoto na Raila Odinga kulia, Machi 25 wakiwa katika mkutano wa kisiasa jijini Nairobi RailaOdingaKE
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa viongozi wa muungano huo na aliyekuwa Makamu wa rais Kalonzo Musyoka amesema, muungano huo hautakubali udanganyifu katika Uchaguzi huo.

Musyoka amesema wamechukua hatua hiyo kwa sababu ni mbinu ambayo imeonekana kufanikiwa nchini Ghana.

Akiwahotubia wafuasi wa upinzani mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Nairobi, Kalonzo amesema hawatakubali wizi wa kura.

Hata hivyo, wanasiasa wa chama tawala cha Jubilee wakiongozwa na Naibu rais William Ruto wamelaani uamuzi huo wa upinzani na kusema kuwa haikubaliwi.

Ruto amewataka wanasiasa hao kuwa na imani na Makamishena wa Tume ya Uchaguzi na kuwalaumu wapinzani kwa kusababisha Makamishena wa zamani kuondoka madarakani kwa kile alichosema hakuwakufanya kosa lolote.

Naibu raia wa Kenya William Ruto akiwa katika mkutano wa kisiasa Machi 25 2017 mjini Naivasha
Naibu raia wa Kenya William Ruto akiwa katika mkutano wa kisiasa Machi 25 2017 mjini Naivasha williamsamoei

Joto la kisiasa nchini kenya limeendelea kupanda wakati huu upinzani ukisubiriwa kumtangaza mgombea wale atakayepambana na rais Uhuru Kenyatta.

Miongoni mwa wanasiasa wanaotafita tiketi ya muungano wa upinzani ni pamoja na Raila Odinga kiongozi wa chama cha ODM, Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper, Musalia Mudavadi wa Chama acha ANC na Moses Wetangula wa chama cha FORD Kenya.