Pata taarifa kuu
BURUNDI

Burundi yalaani wimbo wa Imbonerakure dhidi ya wafuasi wa upinzani

Kulingana na ripoti ya HRW , vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure,  walishiriki katika mauaji ya kikatili mkoani Cibitoke kati ya Desemba 30 na Januari 3.
Kulingana na ripoti ya HRW , vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure, walishiriki katika mauaji ya kikatili mkoani Cibitoke kati ya Desemba 30 na Januari 3. Desire Nimubona/IRIN/www.irinnews.org

Serikali ya Burundi imelaani mkanda wa video unaosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini humo ukiwaonesha wafuasi wa rais Pierre Nkurunziza wakiimba wimbo wa kujisifia kuwa wamewapachika  mimba wanawake na wasichana kutoka vyama vya upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Mkanda huo wa dakika mbili unawaonesha vijana hao wanaofahamika kama Imbonerakure wakiimba kwa Kirundi wakidai kuhusika na ujauzito wa wapinzani hao.

Katika wimbo huo, vijana hao wanasikika wakisema kuwa, wanawake hao wa upinzani watajifungua wafuasi wengine wa Imbonerakure.

Serikali ya Bujumbura imelaani wimbo huo na kusema, lugha iliyotumiwa haiendani na sera na tamaduni ya chama tawala CNDD FDD.

Uchunguzi unaendelea kubaini kwa udani kuhusu wimbo huu, huku serikali ikisema itawachukulia hatua wahusika.

Hii ndo mara ya kwanza kwa kundi hili kushutumiwa hadharani na serikali licha ya kutetewa katika siku zillizopita kuhusu madai ya kuhusika na uhalifu dhidi ya wanawake na wapinzani wa serikali.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, mwaka 2016 liliwashtumu vijana hao wa chama tawala kuwabakla wanawake nchini humo. Unaweza kusoma zaidi katika makala haya.

Burundi imekuwa ikishuhudia mzozo wa kisiasa tangu mwaka 2015, baada ya rais Piere Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu na hata kuzua jaribio la kumpindua.

Machafuko nchini humo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 500 na zaidi ya 200,000 wakikimbilia mataifa jirani.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.